Baadhi ya wanawake Mashuhuri wanaomtangaza Kristo Nchini
kwenye Biblia
kuna orodha ndefu ya wanawake waliosimamia makusudi ya Mungu katika
Mazingira na vipindi tofauti tofauti.Biblia inaonyesha wazi namna
ambavyo kina Debora, Abigaili, Dorcas, Esta na wengine wengi.Hapa nchini
wapo wanawake WENGI wanaoutangaza Ufalme wa Mungu kwa utukufu wa
Mungu.Baadhi ya wanawake ni kama ifuatavyo
Mama Catherine Abihudi
|
Mch Catherine Abihudi
Mch
Catherine Abihuni ni mtumishi wa Mungu ambaye kwa sasa anamtumikia
Mungu akiwa nchini Marekani pamoja na Mumewe Mch Charles Abihudi.Kabla
ya kwenda marekani alikuwa ni mmoja kati ya wanawake waliogusa mioyo ya
watu wengi nchini kwa ujasili wake na uwezo wa kufundisha Neno la Mungu
with revelations.
Amekuwa
akisaidia sana Vijana wa vyuoni na Makanisani na kwa sasa akishirikiana
na watumishi wengine huandaa Makongamano ya Pasaka nchini
Marekani.Kabla ya kwenda Marekani yeye na mumewe walikuwa wakihudumu
katika kanisa la Calvary Asemblies of GOD lililoko chini ya Apostle
Danstan Maboya
Alice Prosper Ntepa Mtoto wa Mama Prosper Ntepa
|
.
Mama Prosper Ntepa
Mama
Mchungaji na mke wa mtumimishi wa Mungu Prosper Ntepa,mama Ntepa kwa
muda mrefu sasa amekuwa mchungaji na ameandaa semina nyingi za kimungu
zenye lengo la kumbomboa mwanamke.Tofauti na kuhubiri madhabahuni Mama
Ntepa anaaminika ndiye Mtumishi wa Kwanza mwanamke nchini kuandika
vitabu vingi vinavyohusiana na maisha ya ukristo.
Mama Kimaro |
Mama Kimaro wa Mwanza
Mch
Mama Kimaro wa huduma ya Divine Favour iliyoko Nyakato jijini Mwanza,
ni mmoja kati ya wamama walioamua kuingia kwenye huduma.Kabla ya
kuanzisha Divine Favour Mama Kimaro alikuwa Mchungaji chini ya Huduma ya
Cathedraw of Joy inayoongozwa na Askofu John Komanya.
Mch Getrude Rwakatare |
Mama Getrude Rwakatare
Mama
Getrude Rwakatare ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B
Asemblies of GOD(Mlima wa Moto).Pamoja na kufanya mengi nchini, Mama
Rwakatare amechunga kanisa kwa muda mrefu sasa na amekuwa ni Mchungaji
wa Kwanza Mwanamke kuingia Bungeni kama Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Mama Diana Mwakasege |
Mama Diana Mwakasege
Ni
wazi kuwa kukua na kufanikiwa kwa huduma ya Mwl Christopher Mwakasege
kwa kiasi kikubwa kumetokana na Ufanisi na jitihada za ubavu wake mama
Diana Mwakasege.Amekuwa mstari wa mbele kuwaleta watu kwa YESU,
kufundisha semina za Vijana na Ujana pamoja na kuwaombea Roho mtakatifu
wale wote wenye kiu ya kujazwa Roho wa MUNGU na MUNGU amekuwa
akionekana katika Maombezi hayo.
Dada Mary Damian |
Mary Damian
Mtumishi
Mary Damian huyu ni binti na mmiliki wa Blog ya kwanza maarufu nchini
iitwayo STRICTLY GOSPEL. Miaka kadhaa iliyopita alianzisha blog hiyo
ambayo imewagusa wengi nchini kwa mijadala na uchambuzi wa kina wa Neno
la Mungu pasipo kujali udhehebu.Kwa sasa Mary yuko Masomoni nchini
Marekani.
Mama Mchungaji Debora Kaisi |
Mama Debora Kaisi
Kwa
watu wanye historia ya kutosha kuhusu Manzese uwanja wa fisi watakuwa
wanajua nini kilikuwa kinafanyika katika viwanja hivyo, palikuwa ni
mahali ambapo starehe za kila aina with cheap Price zilikuwa zikifanyika
kwa viwango vya juu.Unywaji wa pombe zote za kienyeji pamoja na
biashara ya ukahaba vilikuwa vimeweka kambi mahali hapo. Mch Debora
Kaisi na mumewe waliliona hilo na hivyo kuingia kazini kwa kumsihi Roho
wa Mungu alibadilishe eneo hilo.
Mama
Kaisi na mumewe kwa sasa wamefungua kanisa mahali hapo na watu
wanamuabudu Mungu na kwa hili Hosanna Inc tunasema ni EBENEZER.Kwa sasa
hapaitwi tena uwanja wa Fisi bali panaitwa UWANJA WA SIFA.Tofauti na
hayo amekuwa akiendesha semina mbalimbali za mabinti na wanawake
kanisani kwake na katika makanisa mbalimbali.
Dada Rose mushi |
Rose Mushi
Dada
Rose mushi ni mtumishi wa mungu kijana ambaye amebadilisha fahamu za
watu wengi kwa kutumia vitabu.Mpaka sasa ameandika vitabu takribani
vitano vinavyoelezea general things kwenye jamii kwa mlengo wa
bIblia.Vijana wengi nchini wana-potential nyingi ila hawataki ku-dig
deep into their potentials na mwisho wa siku hizo precious potentials
zinapotea.Dada Rose Mushi ameliona hilo na vitabu vyake vimekuwa baraka
kwa wengi na kwa kanisa kwa ujumla.
Mama Lilian Ndegi |
Mch Lilian Ndegi
Mama
Lilian Ndegi ni mke wa Apostle Onesmo Ndegi wa huduma ya Living Water
Kawe Makuti. Kwa muda mrefu sasa amekuwa akiendesha semina za neno la
Mungu zinazohusu Wanawake kwa ushirikiani mkubwa wa watumishi
wengine.Amekuwa bega kwa bega katika kuaendesha semina hizo kwa
ushirikiano wa Mama Ntepa,na mama Debora Kaisi Pamoja na wengine wengi.
Mama Tedy Kwilasa
Ni
vigumu sana kumsahau huyu Mama,Mama kwilasa anaongoza huduma ya Victory
Ministry yenye makao yake makuu jijini Dar es salaam. Kwenye marketing
kuna neno la Kimaketia linaitwa “Marketing Segmentation” na Kimungu kuna
kitu kinaitwa “Centre of the Vision”.Mama kwilasa kwa sehemu kubwa
amebase(segment/centre of her vision ni) kwa wadada.Amekuwa akiendesha
semina nyingi za wadada katika vyuo mbalimbali na ni Mmoja kati ya
Wamama wanaohubiri katika Mikutano ya Nje.
You might also like:
No comments:
Post a Comment