Friday, April 20, 2012

kitabu kwa vijana wanaotakarajia kuo/kuolewa karibuni by pastor dickson mangole




HAPA NI MAELEZO YA KITABU




Kinga na dawa ya mapenzi



                                                                           



Uchumba hadi ndoa





Penzi lilochakaa laweza kuwajipya, na penzi changa laweza kudumishwa
         

Kisomwena wenye umri
Unaowaruhusukuingia
Katika uchumba au ndoa au
Wanandoa


ISBN. 978-9987-9416-2-9


Mchungaji Dickson Mangole







Kitabukimeandikwa na Mchungaji na Mwalimu na Muinjilisti Dickson A. Mangole wa hudumaya Mahanaim Genuine Christians iliyoko Dar es salaam Tanzania
P.o.box 17512 Dares salaamu Tanzania
mobile phones +255 755 528 965/+255 717 528 272 Kenya piga +254 717 232 462
e-mail gmahanaimu@yahoo.com website, http://www.mahanaimgc.webs.com/
Face book. Dickson Mangole

Edited by Jimy Mwaikokesya
Printed by Emac express printing co, Dar es salaam
Toleo la kwanza mwaka 2/23/2012


Haki zote zimehifadhiwa hairuhusiwi kunakili kitabu hiki aukuchapisha kwa njia yoyote bila ya idhini ya Mwandishi na mmiliki wa kitabuhiki Mchungaji D.A. Mangole







Yaliyomo.

i. Utangulizi

1 Penzi ni kitu gani

2 Muda muafaka wa kuindaa ndoa

3 Mbinu za kupata mchumba sahihi

4 Sababu kadhaa zinazo sababisha kukawia kuoa au kuolewa

5 Jinsi ya kulilinda penzi wakati wa uchumba

6 Mahusiano ya uchumba yaliyoharibika

7 Madhara ya ngono (uasherati) kabla ya ndoa

8 Kinga ya mapenzi katika ndoa

9 Kulirejesha penzi lililochakaa aukuharibika

10 Dawa ya mapenzi katika ndoa

11 Mbinu ya kumuathiri mwenzi wako kimapenzi (affect)

12 Malingo ujanani uzeeni ni vituko

13 Kuwa na wasiwasi wa mapenzi

14 Tendo la ndoa ni tiba

15 Kujua vinavyopendwa na mwenzi wako

16 Madhara ya kuachana

17 Muongozo wa umilikaji mali kwa wanandoa

18 Mirathi (urithi) kwa mujibu wa Biblia

19 Uzazi wa mpango kwa mujibu wa Biblia

21 Maoni ya msomaji

22 Mithali za DicksonMangole

23 Bidhaa zangu


i. Utangulizi

Kitabu kimeandikwa na kutolewana mchungaji Dickson Mangolewa huduma ya Mahanaim Genuine Christians Pentecostal Church. Iliyoko Dar es salaam Tanzania
 Yeye ni mchungaji namwalimu na muinjilisti wa kimataifa

Yeye amekuwa na uzoefu wa maisha ya ndoa zaidi ya miaka 17hadi kitabu hiki kinapokufikia; Pia amekuwa mshauri wa ndoa kwa miaka mingi,amerekebisha ndoa nyingi zilizokaribia kuharibika 

Pia ni mwalimu wa vijana, yeye anahuduma ya kuwasaidiavijana hasa katika kuishi maisha ya kuvishinda vishawishi vya shetani nakuwafundisha namana ya kupata wachumba kwa njia sahihi, wengi wamesaidika

kulingana na ufundi na umahili wa uandishi wa mtumishi waMungu huyu hakika hatujutia kuwa na kitabu hiki, ukweli ni kwamba kuna wengiwanaandika bali kuna wenye vipaji vya pekee katika kuandika na mmoja wahao nimtumishi wa Mungu Dickson Mangole, yeye huwa anaujuzi wa kupanga mada zake vizurikiasi kwamba hata kama ukiwa mvivu wa kusoma utaweza kusoma vitabu vyake bilaya kukuchosha

kitabu hiki ni cha tatu kuandika, cha kwanza kinaitwa Ufunguo wa kuzungumza na Waislamu; chapili kinaitwa. Uchumi huru usiokuwa na majuto. Na cha tatu nihiki kinachoitwa, Kinga na dawa yamapenzi.

Usishangazwe kuona huyu mchungaji kuandika mambo kuhusu ndoa,uchumba,  na mapenzi, hii alifanya kwamakusudi baada ya kufanya utafi wake kuona eneo hili limeachwa kuzungumziwa kwakina,  na matatizo mengi ya kijamii huwayanaanza hasa pale watu wanapokosa maelekezo sahihi yahusuyo maisha ya ndoa.

Na namna gani mtu atafanya uamuzi sahihi wa kujua ni yupianafaa kuwa mwenzi wake katika ndoa, shida ya ndoa nyingi huwa zinasababishwana uamuzi mbaya wa kuchagua mchumba, mara nyingi wengi wao huwa hawajui kanuniya kutafuta mchumba, wengi huwa wanafuata msisimko wa mapenzi badala yakuchunguza hali harisi

Fuatana na mtumishi wa Mungu huyu hatua kwa hatua


1Penzi ni kitu gani ?

Hakuna lugha sahihi ya kukidhi maana ya neno hili kulinganana uzito wa maana iliyomo ndani ya neno hilo

Hapa nitatoamaana  kadhaa ya neno penzi au mapenzi

1 Unaposema mapenzi au penzi ina maana ya kufurahia, aukupenda yaani kwa kiingereza (love)ina maana ya. Upendo, huba, mapenzi, mahaba, be in love with, penda mwanamke au mwanamume

2 Mapenzi ni raha iliyopindukia mipaka 

3 Mapenzi ni kumpa thamani ya pekee mwenzi wako, ambayothamani kama hiyo huwezi kumpa tena mtumwingine ila yeye tu

4 Mapenzi ni sifa maarumu waliyonayo watu wawili yaani mke namume

5 Mapenzi nimatendo yanayo sababisha mapenzi yawepo

6 Mapenzini utamu mtupu

7 Mapenzini ni kama kifo cha roho na nafsi na mwili, maana kama mapenzi humfikishamahali mtu kupoteza uwezo wa kuwaza kitu kingine au kushindwa kuona kasoro ya mwenziwake, sio hivyo tu hata kuthubutu kuwaacha baba yake na mama yake na ndugu zakena kuambatana na mwenzi wake

Hili sio jambo lakawaida, hiki mimi nakiita ni kifo cha mapenzi au nafananisha mapenzi na kifo,kwasababu mtu anayekufa huwa hana uwezo wa kukumbuka au kuwaza kitu chochote.Soma Mwanzo 2:24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe,nao watakuwa mwili mmoja.


2 Muda muafaka wa kuindaa ndoa

Siku zetu za leokumekuwa na shida kubwa hasa katika maisha ya ndoa, kumekuwa na migogoromikubwa, na machafuko pamoja na magomvi hadi na vifo, na hata kuachana, ndoakukosa amani.

Likini sababuyake kubwa inatokana na kushindwa kujua mudamuafaka wa kuindaa ndoa; maana siri au msingi wa ndoa bora na imara iliyojaa amani ni malezi mema yenye maadili sahihi yenye adabu

Siku zetu za leojamii imepoteza malezi na maadili na ndio imekuwa  chanzo cha kuwa na ndoa mbovu

Ili kuwa na ndoaimara ni lazima tujue ndoa haiandaliwi kwenye kicheni pati nk. Sio rahisikuiandaa ndoa baada ya mume au mke kupata mchumba, hilo ni jambo lisilowezekana

Ndoa inatakiwakuandaliwa hasa na wazazi, kumuandaa mtoto wako toka akiwa mdogo kwakujua sikumoja mtoto wako ataingia katika maisha ya ndoa, sasa, inabidi kumuwekea msingiutakao muwezesha kuingia na kuishi katika maisha ya ndoa, na kumuepushaasiingie kwenye matatizo ambayo yanaweza kuepukika, kuna mithali isemayo “samaki mkunje angali mbichi”

Kwa kawaida ndoainatakiwa kuandaliwa tangu mtoto wa siku moja akiwa bado ana nyonya, unaaza naehapo hapo kwenye ziwa kuamuandalia maisha yake ya  ndoa kwa kumshikisha adabu kwa kumfinya paleanapong`ata titi anapo nyonya

Mtoto hatakiwakulelewa maisha ya kudekezwa ni hatari sana, mtoto aonywe na aadhibiweanapokosea. Mithali 23:13.14 Usimnyime mtoto wako mapigo; maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Utampigakwa fimbo, na kumuokoa nafsi yake na kuzimu

Kumuonya mtoto wakoni agizo la Mungu. Waebrania 12:7.11 Ni kwaajiliya kurudiwa mwastahamili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwana babaye? Basi mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwawana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. Na pamoja na hayo tulikuwa nababa zetu wa mwilini walioturudi, nasi tukawastahamili, basi si afadhali sanakujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? Maana ni hakika, hao kwasikuchache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ilituushiriki utakatifu. Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa  kitu cha furaha, bali cha hudhuni; lakinibaadae huwaletea wale walio zoezwa nayo matunda ya haki yenye amani 

Mithali 22:6 Mleemtoto katika njia impasayo, naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

Kwa mujibu wamaandiko tuliyo soma hapo ju; tunajifunza iwapo watoto watalelewa vizuri basiwataendelea kuwa na tabia njema hadi uzeeni, ni lazima tukiri matokeo ya ndoambovu ni matokeo ya malezi mabaya, maana ndoa inahitaji tabia njema, namatatizo yaliyomo katika ndoa kwa asilimia kubwa yanasababishwa na tabia mbayaambazo si za kiutu

Pia watotowafundishwe kufanya kazi za mikono nyumbani wanaume wajue kufanya kazi zamikono, na wasichana pia wasiwe ni wakukaa tu bali wafundishwe kutunza nyumbamfano kupika kufua nguo, kutandika kitanda,

Kuwa na uwezo wakuitunza nyumba kwa ujumla, leo hii tuna wasichana ambao hawajui hata kuchemshachai, hii ni hatari kwa jamii yetu, tutawapeleka wasichana wetu katika maishaya ndoa  hali hawajui, a, wala be, 

Namalizia kwakusema kuwa muda muafaka wa kuindaa ndoa ni kuanzia pale mtoto akiwa mdogo,yaani kumpa malezi muafaka yatakayo mfanya kuwa na tabia inayofaa kwenye maishaya ndoa


3 Mbinu za kupata mchumba sahihi

Kumpata mchumbasahihi sio jambo rahisi, ni lazima uwe na maarifa na uelewa ili umpate
Hasa kwa wanawake,pengine licha ya vigezo lakini pia unatakiwa kuwa na mbinu kadhaa za kumuingizamtegoni mwanamume umtakaye awe mchumba wako,

Mbinu ninayoizungumzia  ni kumfanya avutiwe na wewe,au apate sababu ya kumfanya akubali wewe uwe mchumba wake, nasema hivi kutumiambinu halali sio kosa, jambo la msingi usijiingize kwenye dhambi

Pengine hatakumtamkia mwanamume kuwa unampenda na kama ataona vema akuoe kwa ndoa takatifu,kwakusema hivyo hakuna ubaya, na usimwambie roho kasema, au nimeonyeshwa naBwana, usiseme uongo, sema tu nimekupenda na kama na wewe utaona vema, basituoane, na usipoona vema basi

Hii ni kwasababubaadhi ya wanaume wengine huwa hawawezi kumtakia mwanamke kwa sababu ya aibu, sasaiwapo utamtakia utakuwa umemsaidia, mara kadhaa ilitokea
kijana au mwanamumeanamtaka mwanamke fulani, lakini anashindwa kusema, utadhani hana mpango nae,kumbe anashindwa jinsi ya kumuanza, au hajui ni hatua ipi ya kuichukua iliujumbe wake ufike

Sasa iliwahikutokea mwanamume mwingine akajitokeza na kuongea na yule mwanamke naakakubaliwa, na baadae yule mwanamume aliyeshindwa kusema, akaanza kukasirikakuona mwenzake amempata, sasa hii  ndiosababu wanawake mara nyingine nimeshauri msione kuwa shida kumtakia mwanamume  akuoe, na mara nyingi ni rahisi kumgunduamwanamme anayekupenda ila anashindwa kutamka, utona tu dalili fulani

Kumbuka Munguameviweka vitu vyote kwa ajili yetu isipokuwa ni sisi tutumie mbinu fulani ilituvichukue na kuwa mali yetu

Mambo kadhaa ya kuyazingatia ili kupata mchumba sahihi

Ukitaka upatemchumba sahihi ni lazima na wewe uwe sahihi, kwani, kama wewe mwenyewe  hauko sahihi sio rahisi kumpata mchumbasahihi, na hata ukimpata huyo mchumba sahihi wewe utakuwa wa kwanza wakumuharibu

Vigezo vya muhimu vya mchumba sahihi

1  Nimuhimu sana uwe unamjua vema huyo mtu, nina maana hii, ujue historia yake,miaka yake ni mingapi, aliwahi kuoa au kuolewa, kabila yake, desturi za kabilaau ukoo wake, tabia zake nzuri ni zipi na mbaya ni zipi, hana magonjwa hatari,anafanya kazi gani, sio mzinzi,? Na nivema umchunguze bila ya yeye kujua, nahata kama umegundua baadhi ya tabia zake zilizo mbaya, lakini iwapo yale memayanazidi mabaya hakuna ubaya wa kuoana naye, na iwapo atakamilisha vigezo vilevya muhimu

Umri sio tatizokubwa, tatizo ni vigezo vya muhimu, ijapokuwa mara nyingi hasa kwa wanaume ninjema zaidi kuoa mwanamke ambae umemzidi umri yaani mwanamume awe ana umrimkubwa kidogo kuliko mwanamke, lakini isiwe ni kigezo kikubwa kikakufungapengine angalia zaidi vigezo muhimu, iwapo utalazimika kumuoa mwanamke mwenyeumri mkubwa kuliko wako

Na mwanamke piahakuna tatizo iwapo utaolewa na mwanamume mwenye umri mkubwa iwapo amekupendana anavigezo unavyo vitaka, au pengine pia ikatokea mwanamume anayetaka kukuoaana umri mdogo lakini amekupenda isiwe tatizo iwapo ana vigezo vinavyo hitajika

2 Awe na imani sawa na yako hasa kama mkristo uliyeokoka na unayempendaYesu, ni vema uolewe na mume mwenye imani moja na yako. Mwanzo 24:1.9 Utaona Ibrahimu alipotaka mwanawe Isaka aoe akaagiza aende kuoa kwa watu wanyumbani kwake sio kwa binti za Wakanaani

3 Awe na tabia njema

4 Akupende kwa dhati

5 Kwa upande wawanawake usiweke kigezo cha kuolewa na mwanamume tajiri tu bali hata kama sio tajiri lakini awe muhangaikaji

6 Awe tayari kufuatautaratibu wa ndoa, ikiwemo pamoja na kukubali kujitokeza kwa wazazi wako na kujitambulisha,na kuomba apewe utaratibu wa kuoa kwa mujibu wa jamii yao, baada ya hayo bilaya kupoteza muda akubali kumuona kiongozi wenu wa kiroho, yaani mchungaji nk.Awepe utaratibu wa uchumba na ndoaili mjue unakuwaje, na kama wazazi wenu hawajaamini, basi itakuwa ni vema kumuona mchungaji wenu hata kabla ya wazazi

Kumbuka uchumbasahihi ni ule wa kuahidiana tu kuwa iwapo mtakamilisha taraibu za kufunga ndoamtakuwa mke na mume, na wakati mkiwa katika mchakato wa uchumba hairuhusiwi kujamiiana kabla ya ndoa takatifu

Maana ndoa inakamilishwa na tendo la kujamiana, mkisha jamiianahuo hauitwi tena uchumba, baliitaitwa ni ndoa haramu,  mkisha jamiianatu itahesabika mmejifungisha ndoa isivyo halali.

Hivyo mtakuwa hamna radhi kwa wazazi na hata kwa kanisa laMungu

7 Katika njia zote lakini pia iliyo muhimu zaidi ni yakumuomba Mungu akuongoze kumpata mchumba aliye sahihi, Biblia imetuonyatusitengemee zaidi akili zetu, bali tumtumaini Mungu kwa mioyo yetu yote Mithali 3:5.6

8 Iwapo utautilia shaka uchumbawenu basi ni jukumu lako kufanya utafiti wa kina ili ujiridhishe; Na kama kunajambo linaashiria hofu fulani usilazimishe kufunga ndoa katika mazingira yanamna hiyo, bali songeza kwanza muda wa kufunga ndoa mbele na iwapo bado kunasimtofahamu, basi vunja uchumbamapema, maana ndoa sio jambo la kubahatisha, na bora kuvunja uchumba kuliko kuingia katika ndoahalafu ukawaza kutoka na usiweze


2 Muda muafaka wa kuindaa ndoa

Siku zetu za leo kumekuwa na shida kubwa hasa katika maisha ya ndoa, kumekuwa na migogoro mikubwa, na machafuko pamoja na magomvi hadi na vifo, na hata kuachana, ndoa kukosa amani.

Likini sababu yake kubwa inatokana na kushindwa kujua muda muafaka wa kuindaa ndoa; maana siri au msingi wa ndoa bora na imara iliyo jaa amani ni malezi mema yenye maadili sahihi yenye adabu

Siku zetu za leo jamii imepoteza malezi na maadili na ndio imekuwa chanzo cha kuwa na ndoa mbovu

Ili kuwa na ndoa imara ni lazima tujue ndoa haiandaliwi kwenye kicheni pati nk. Sio rahisi kuiandaa ndoa baada ya mume au mke kupata mchumba, hilo ni jambo lisilowezekana

Ndoa inatakiwa kuandaliwa hasa na wazazi, kumuandaa mtoto wako toka akiwa mdogo kwakujua siku moja mtoto wako ataingia katika maisha ya ndoa, sasa inabidi kumuwekea msingi utakao muwezesha kuingia na kuishi katika maisha ya ndoa, na kumuepusha asiingie kwenye matatizo ambayo yanaweza kuepukika, kuna mithali isemayo ?samaki mkunje angali mbichi?

Kwa kawaida ndoa inatakiwa kuandaliwa tangu mtoto wa siku moja akiwa bado ana nyonya unaaza hapo hapo kwenye ziwa kuamuandalia maisha yake ya ndoa kwa kumshikisha adabu kwa kumfinya pale anapong`ata titi anapo nyonya

Mtoto hatakiwa kulelewa maisha ya kudekezwa ni hatari sana, mtoto aonywe na aadhibiwe anapokosea. Mithali 23:13.14 Usimnyime mtoto wako mapigo; maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa. Utampiga kwa fimbo, na kumuokoa nafsi yake na kuzimu

Kumuonya mtoto wako ndio agizo la Mungu. Waebrania 12:7.11 Ni kwaajili ya kurudiwa mwastahamili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? Basi mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwilini walioturudi, nasi tukawastahamili, basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? Maana ni hakika, hao kwasiku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu. Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha hudhuni; lakini baadae huwaletea wale walio zoezwa nayo matunda ya haki yenye amani

Mithali 22:6 Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

Kwa mujibu wa maandiko tuliyo soma hapo ju; tunajifunza iwapo watoto watalelewa vizuri basi wataendelea kuwa na tabia njema hadi uzeeni, ni lazima tukiri matokeo ya ndoa mbovu ni matokeo ya malezi mabaya, maana ndoa inahitaji tabia njema, na matatizo yaliyomo katika ndoa mengi ya hayo yanasababishwa na tabia mbaya ambazo si za kiutu

Pia watoto wafundishwe kufanya kazi za mikono nyumbani wanaume wajue kufanya kazi za mikono, na wasichana pia wasiwe ni wakukaa tu bali wafundishwe kutunza nyumba mfano kupika kufua nguo, kutandika kitanda, kuwa na uwezo wa kuitunza nyumba kwa ujumla, leo hii tuna wasichana ambao hawajui hata kuchemsha hata chai, hii ni hatari kwa jamii yetu, tutawapeleka wasichana wetu katika maisha ya ndoa hali hawajui, a, wala be,

Namalizia kwa kusema kuwa muda muafaka wa kuindaa ndoa ni kuanzia pale mtoto akiwa mdogo, yaani kumpa malezi muafaka yatakayo mfanya kuwa na tabia inayofaa kwenye maisha ya ndoa
Reply Pastor Dickson Mangole
02:46 AM on March 05, 2012 
UZINDUZI UMEISHA SALAAMA

1 comment:

  1. Rangi ya maandish inaumiza macho, mfanyie research hilo suala..!!

    ReplyDelete