Friday, April 20, 2012

 

CHANGAMKA KUWAPENDEKEZA WAIMBAJI WA GOSPEL TANZANIA KWENYE TUZO ZA AFRIKA NCHINI UINGEREZA

Ukumbi ambao kutafanyika tuzo hizo mwaka huu.
                                 
                                                                www.africagospelawards.com
hii ni kwa mujibu wa GOSPELKITAA.BLOGSPOT.COM

Zoezi la upendekezaji wa waimbaji watakaopigiwa kura kuwania tuzo za African Gospel Music Award 2012 zinazotarajiwa kufanyika mwezi wa saba jijini London nchini Uingereza,linatarajia kuanza kesho tarehe 21 hadi tarehe 21 mwezi May 2012.

Kutangazwa kuanza kwa zoezi hilo ni kama lamgambo limelia kwa watanzania kuamka na kuanza kupendekeza waimbaji ambao wanajua watafanya vizuri na kupata tuzo hizo ambazo pia zitasaidia kuwatangaza nje ya mipaka ya Tanzania na kufungua milango ya kupata mialiko ya kwenda kuhudumu sehemu nyingine duniani kama ilivyo kwa waimbaji wa nchi jirani ya Kenya ambao tayari wameanza kujulikana vyema nje ya nchi yao.

Mashindano hayo yaliyoanza rasmi mwaka 2009 yamezidi kupata umaarufu kila mwaka,ambapo mwaka jana mwimbaji Christina Shusho alipendekezwa lakini kura hazikuwa za kutosha kupata tuzo.katika tuzo za mwaka huu waimbaji mbalimbali wataimba wakati wa utolewaji wa tuzo hizo akiwemo mwanadada Emmy Kosgei wa Kenya,Mkhululi Bhebhe wa Joyous,Atta Boafo aliyeimba remix ya My God is good,pia kati ya washereheshaji wa tuzo hizo ni mwanakaka mwenye sauti ya kipekee mwenye asili ya Ghana mwenye makazi yake nchini Uingereza Sonnie Badu.

            ILI KUWEZA KUWAPENDEKEZA WAIMBAJI INGIA KWENYE TOVUTI HII
                                                        www.africagospelawards.com

ukiingia ndani ya tovuti hiyo utapata maelekezo ya namna ambavyo unaweza kuwapendekeza waimbaji.                                    






No comments:

Post a Comment