NAFASI YA MWANAMKE KIBIBLIA.
Na; Patrick samson Sanga.
Mwanzo 1:27 ‘Mungu akaumba mtu kwa mfano wake,kwa mfano wa Mungu
alimwumba,mwanaume na mwanamke aliwaumba. Sikiliza mahali popote pale
mwanamke ni mtu mwenye nguvu na ushawishi mkubwa katika kufanya mambo
kuliko hata mwanaume.Ikiwa ushawishi huu utatumiwa katika mpango wa
Mungu basi kusudi la Mungu litatekelezwa.
Mungu hakumwumba mwanamke kwa bahati mbaya au makosa,kila ambacho
Mungu alikifanya ,alikifanya kwa kusudi.kwa lugha nyingine kila ambacho
Mungu alikifanya maana yake moja kina nafasi mbele zake na mbili kuna
wajibu ambao Mungu aliweka ili utekelezwe na hicho kitu.
Lengo la ujumbe huu ni kukueleza nafasi ambayo Mungu amempa mwanamke
katika kanisa,jamii,nchi,ndoa na nk na wajibu wa yeye kutekeleza katika
nafasi hiyo:-
1.Mungu anamtazama mwanamke kama msaidizi wa mumewe .
Mwanzo 2:18 “Bwana Mungu akasema si vyema huyo mtu awe peke
yake,nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye”. Tangu kuumbwa kwa
Adam,mpaka Mungu kumletea Eva inasemekana miaka mingi ilipita hapa
katikati.Sasa tunajua katika ile sura ya kwanza na ya pili ya kitabu cha
mwanzo,Mungu alikuwa amempa Adam wajibu wa kutekeleza.
Ikafika wakati Mungu akaona ule wajibu ni mkubwa sana kwa Adam
kuutekelekeza ndipo akampa Eva.Kitu Mungu anataka tujue hapa ni
hiki,wajibu aliopewa Adam peke yake asingeweza kuutekeleza bila
Eva,maana yake nafasi ya Eva kwa Adam ilikuwa ni ya muhimu zaidi.Pasipo
Eva,Adam angeshindwa kutekeleza wajibu.
Sasa hata leo katika ndoa,kanisa Mungu ameweka wanawake ili wawe
wasaidizi katika majukumu ambayo Mungu amewapa na waume zao au
wachungaji wao makanisani.
2. Mwanamke kama mlinzi wa agano na kusudi la Mungu. Mithali 14:1 “ Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake ; bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe” , Mwanzo 3;13 “ Bwana Mungu akamwambia mwanamke ,nini hili ulilolifanya ? Mwanamke akasema nyoka alinidanganya ,nikala”..
2. Mwanamke kama mlinzi wa agano na kusudi la Mungu. Mithali 14:1 “ Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake ; bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe” , Mwanzo 3;13 “ Bwana Mungu akamwambia mwanamke ,nini hili ulilolifanya ? Mwanamke akasema nyoka alinidanganya ,nikala”..
Ndoa ni agano la Mungu kwa wanadamu. Mlinzi wa agano kimsingi ni
mwanamke. Mara nyingi shetani akitaka kuvuruga ndoa atatafuta mpenyo au
nafasi hiyo kwa mwanamke ili asambaratishe ndoa hiyo.Sasa mwanamke yupo
ili kulinda kusudi hilo.Asipokaa kwenye nafasi yake ya ulinzi basi ajue
kwamba kusudi la Mungu la kuwaunganisha halitatimia.
Nisikilize ndoa yoyote inapovuruguka ujue mwanamke hakusimama vema
kwenye nafasi yake ya ulinzi. Ngoja nikuonyeshe kitu hiki. Adam na Eva
walipokula tunda ambalo Mungu aliwaambia wasile , kila mmoja wao
aliulwiza swali lake. Adamu aliulizwa uko wapi? Mwanzo 3:9, na Eva alimwambia Mwanamke ni
nini hili ulilolifanya , Mwanzo 3:13.Ipo tofauti kubwa sana katika haya
maswali mawili.Swali la Adam lilimaanisha kwa nini haupo kwenye nafasi
yako? Na swali la Eva lilivuka hapo na kumaanisha kwa nini hujafanya
ulilotakiwa kufanya yaani kulinda agano.Mahali popote mwanamke ulipo
ikiwa ni katika ndoa ,kanisa ,jamii,nchi, jifunze kulinda kusudi la
Mungu ambalo unajua Mungu amekuagiza . jifunze kupitia mama yake Musa ,
yeye alilinda agano la wana wa wa Israeli kwa kumficha Musa na
kuhakikisha hafi maana alijua Musa hakuzaliwa kwa bahati mbaya. Kutoka
2:1-10.
3.mwanamke kama muombolezaji.
Luka 23;27-28 “Mkutano mkubwa wa watu wakamfuata na wanawake
waliokuwa wakijipiga vifiua na kumuombolezea , Yesu akawageukia akasema
,Enyi binti za Yerusalemu ,msinillie mimi bali jililieni nafsi zenu na
watoto wenu”.Sikliliza , Mungu amweapa kinamama uwezo mkubwa wa
kuomboleza kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ndani ya jamii ,ndoa,
kanisa, nchi nk. Hivyo Mungu anamuhesabu mwanamke kama muombolezaji.
Hii ina maana kam kuna vitu havijakaa sawasawa kwenye
ndoa,kanisa,nchi nk, Mungu anajua mwanamke atasimama kwenye nafasi yake
na kuomba ili Mungu apate kuliponya taifa kupitia maombi .Ukiona maasi
mengi yamezidi katika taifa mfano, vijana wa kike kutoa mimba,
uasherati,uchafu na uzinzi basi ujue kina mama katika mji au taifa
hawajasimama vizuri kwenye nafasi zao. Si kana kwamba nawalaaumu mama
zangu na dada zangu kwa kusema hivyo,bali ninachotaka niwaonyeshe ni
kwamba usalama na maendeleo mazuri ya vijana wa kike na kiume katika
familia,kanisa na taifa kwa ujumla upo katika mikono yenu na ndio maana
Yesu aliwaambia mjililie ninyi na hao vijana wenu.
Nikuulize swali , jiulize una weatoto wangapi? Tabia na mwenendo wao
ukoje? Je ni mzuri? Unambariki Mungu? sivyo jiulize chanzo cha tabia
hizo kwa mwananao ni nini au ni nani aliyehusika na tabia hiyo? Najua
unaweza kwa haraka kusema ni shetani au kumtupia lawama mmeo. Sikiliza
Shatani huwa hafanyi chochote isipokuwa pale anapokuwa amepewa
nafasi na mtu au watu fulani , kwa kifupi mtu anaposhindwa kusimama
kwenye nafasi yake. Sasa ukisoma vizuri Biblia utagundua nafasi ambayo
Mungu amempa mwanamke kwa habari ya watoto wake, ndoa yake, kanisa lake kwa ujumla.
Jifunze kusimama kwenye nafasi yako, funga na kuomba kwa ajili ya
taifa hili ili Bwana Mungu apate kuliponya . maombi yako yatasababisha
kutengenezwa kwa mahali palipobomoka na krejeshwa kwa njia za kukalia.
4.Mwanamke kama mlinzi wa nafsi ya mtoto wake wa kiume .
4.Mwanamke kama mlinzi wa nafsi ya mtoto wake wa kiume .
Katika hii sura ya 31 ya kitabu cha Mithali tunaona habari za mama
mmoja ambaye alikuwa na mtoto wa kiume na huyu mtoto alikuwa ni mfalme.
Ule mstari wa pili unasema “ Ni nini mwanangu ?, tena ,nini mwana wa
tumbo langu? Tena nini mwana wa nadhiri zangu ? Usiwape wanawake nguvu
zako; wala moyo wako usiwape wale waharibuo wafalme”. kinamama wakijua
namna ya kuzikamata nafsi za watoto wao wa kiume ,nakuambia kuna
uwezekano mkubwa kabisa hawa watoto wasifanye tendo la ndoa mpaka
watakapo kuja kuoa.
Hili litawezekana pale tu kinamama watapofanikiwa kuzikamata na kukaa
kwenye nafsi za watoto wao wa kiume.Huyu mama alimuuliza maswali mengi
mwanawe kwa sababu aliona nafasi yake mama kwenye nafsi ya mwanawe
inanyang’anywa na wanawake wengine.
Naamini waraka huu mfupi na wa kwanza utafanyika kuwa msaada kwa wamama wengi mahala popote pale.
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi.
No comments:
Post a Comment