ENYI WANAWAKE MSINILILIE MIMI.
Na; Patrick Samson Sanga.
Kwa nini Yesu aliwaambia akinamama jililieni nafsi zenu na watoto wenu ?
Luka 23:27-28 “Na mkutano mkubwa wa watu wakamfuata na wanawake waliokuwa wakijipiga vifua na kumwombolezea, Yesu akawageukia,akasema,Enyi binti za Yerusalemu ,msinililie mimi,bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu”.
Luka 23:27-28 “Na mkutano mkubwa wa watu wakamfuata na wanawake waliokuwa wakijipiga vifua na kumwombolezea, Yesu akawageukia,akasema,Enyi binti za Yerusalemu ,msinililie mimi,bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu”.
Hapa Bwana wetu Yesu alikuwa njiani kuelekea Golgotha kusulubiwa,
akina mama na binti za Yerusalemu wakawa wanamlilia na kumwombolezea
Yesu kwa uchungu sana.
Sasa kwa kawaida mtu anapokuwa anapita kwenye hali ngumu au matatizo
au msiba au janga lolote zito kwa kawaida tunapenda watu wengine
watufariji na waomboleze pamoja na sisi na ndiyo maana hata Paulo
alisema lieni pamoja na wanao lia nk
Lakini jambo hili halikuwa hivyo kwa Yesu ,kile kilio cha wale akina
mama kilimfanya Yesu awageukie na kutoa ujumbe wa ajabu kwa wale akina
mama na ndipo akasema msinililie mimi,bali jililieni nafsi zenu na
watoto wenu .
Nimeandika ujumbe huu mfupi ili kujibu maswali mawili ambayo
tunayapata kutoka katika sentensi ya Bwana wetu Yesu kwa hawa wamama
nayo ni;
Moja, kwa nini Yesu aliwaambia msinililie mimi ? mbili kwa nini Yesu aliwaambia jililieni nafsi zenu na watoto wenu?. Yesu aliwaambia msinililie mimi kuu mbili nazo ni;
Moja, kwa nini Yesu aliwaambia msinililie mimi ? mbili kwa nini Yesu aliwaambia jililieni nafsi zenu na watoto wenu?. Yesu aliwaambia msinililie mimi kuu mbili nazo ni;
{a}Ili neno liweze kutimia.Yohana 3:16. Mapatano ya Yesu na baba kule mbinguni ilikuwa Yesu aje na afe kwa
ajili ya watu wake. Ili mlazimu Yesu kupita kwenye hiyo njia, hata kama
wangeombolezaje kilio chao kisingeweza zuia kifo cha Bwana Yesu.
Kumbuka kule Gethsemane Ysu mwenyewe aliomba akasema Baba,
ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke, Lakini tunaona Mungu alituma malaika
kumfariji na kumtia moyo na Yesu mwenyewe alikuwa tayari mapenzi ya
Mungu yatimizwe.
{b} Kilio chao kingemhuzunisha na kumvunja moyo zaidi. Matendo ya
Mitume 21:9-14.Hapa ulikuwa umetolewa unabii wa jinsi vile Paulo
atakavyouawa kule Yerusalemu. Na watu wa nyumba ile wakaanza kulia na
kumsihi Paulo asipande kwenda Yerusalemu, Ndipo Paulo akawaambia
mnafanya nnini, kulia na kunivunja moyo?. Kwa hiyo hata Yesu angekutana
na hali ka,a ya Paulo.
Swali la pili; Kwa nini Yesu aliwaambia wamama bali jililieni nafsi
zenu na wato wenu na Je alikuwa ana maana gain kuwaambia hivyo?
Kabla sijakuambia hizo sababu, ngoja kwa kifupi nikuambie habari za nafsi. Kwa kiyunani inaitwa (psuche).Nafsi inahusika kuelekea ndani ya mtu.Ndani ya nafsi ndiko kwenye hisia,akili na maamuzi ya mtu.Hivyo nafsi ya mtu inahusika na maauzi, hisia na nia za mtu binafsi. Nafsi inatabia ya kuugua,kuinama, na na kuumia pale inapojeruhiwa.
Kabla sijakuambia hizo sababu, ngoja kwa kifupi nikuambie habari za nafsi. Kwa kiyunani inaitwa (psuche).Nafsi inahusika kuelekea ndani ya mtu.Ndani ya nafsi ndiko kwenye hisia,akili na maamuzi ya mtu.Hivyo nafsi ya mtu inahusika na maauzi, hisia na nia za mtu binafsi. Nafsi inatabia ya kuugua,kuinama, na na kuumia pale inapojeruhiwa.
Siku zote nafsi inagojea mwongozo wa roho au mwili wa mtu. Mtu akiwa
ni wa rohoni nafsi itakaa mkao wa rohoni na mtu akiwa ni wa mwilini na
nafsi yake itakaa mkao wa mwilini.Nafsi inaishi sasa kwa kutegemea
maneneo unayojisemea au kusemewa na wengine sasa au wakati
uliopita.Hivyo Yesu alipowaambia wale kinamama msinililie mimi alikuwa
na maana hii na sababu hizi;
*Moja, Yesu alijua akinamama wengi ni watu ambao nafsi zao ni rahisi
kujeruhika na kuinama pindi wanapokutana na matatizo mbalimbali na zaidi
kina mama wengi ni watu ambao ni wepesi sana kuijtamkia maneno ambayo
kwa namna moja au nyingine yanajeruhi nafsi na kuharibu future yao
wenyewe.
Kwa Kujua kwamba akina mama wengi mara nyingi huwa wanajitamkia
maneno ambayo yanaathari kwao wenyewe, watoto wao, familia zao, kanisa
lao na hata nchi nk ndio maana Yesu alisema jililieni nafsi zenu.
Alikuwa akimaanisha nini?
Alikuwa akimaanisha nini?
Yesu alikuwa anawaambia wale wamama wajitunze nafsi zao na za watoto
wao kwa kuhakikisha ndani wanweka neno la Mungu linalozungumzia maisha
yao ya baadae (future).
Hili neno litazifanya hisia zao, na akili zao na maamuzi yawe
yatawaliwe na ahadi za Mungu na hii itawasaidia nafsi kutokuinama wala
kujeruhika pindi wanapokutana na matatizo mbalimbali. Neno hili litawapa
jibu la kukabiliana na mazingira ya kila nmana kwa sababu hiyo Jehanamu
itakosa watu .
*Mbili ni kwa sababu ya nafasi na wajibu ambao Mungu amewapa akinamama kama walinzi wa kusudi lake popote pale walipo.
Nisikilize mwanamke Mungu amekuheshimu sana kukupa wajibu wa kulinda
agano na kusudi lake duniani.Shetani anapotaka kuvuruga na kuharibu
kusudi la Mungu mahali popote pale, uwe na uhakika lazima tu ataanza
kutafuta njia na mpenyo kwa mwanamke.Shetani akitaka kuleta vurugu
kwenye ndoa,kanisa,familia uwe na uhakika atafanya kila analoweza apitie
kwa mwanamke.
Hebu chukua dakika moja tafakari vile shetani anavyovuruga vijana wa
kike na wa kiume, kwa kuwafanya mabinti watoe mimba na kuua bila hata
hofu kwa Mungu, Wazazi kufanya tendo la ndoa na wanao, ndugu kwa ndugu,
Yesu aliona huzuni na kilio kikubwa ambacho kwanza kitawapata kinamama
hapahapa duniani na baadaye katika dhiki kuu na mwisho katika Jehnamu ya
moto na ndiyo maana alisema watasema heri wa matumbo yasiyozaa na
matiti yasiyonyonyesha.
Mwanamke hakikisha uniombolozea nafsi na kuiambia nafsi yangu mtii
Mungu, nafsi yangu usiiname kwa yale unayoaona, hawa watoto wangu si ya
dunia, iambie nafsi yako kwamba hawa watoto, hii ndoa, kanisa,
vijana,nchi nk ni ya Bwana .
Hakuna hata mmoja wa watoto wangu watakaokwenda Jehnamu , sizai
watoto wa kwenda Jehanamu nk.Hakikisha ndani yako ahadi za Mungu zinajaa
kwa wingi ili nafsi isitekwe na hivyo ukawa umemruhusu shetani kuvuruga
na kuharibu kusudi la Mungu kupitia wewe .
Naamini ujumbe huu utawasidia wamama wengi Kujua namna ya
kushughulika na nafsi zao na kuhakikihsa haziwafanyi kutoka kwenye
kusudi la Mungu.
Neema ya Kristo na iwe nawe.
No comments:
Post a Comment